Tuesday, May 24, 2016

AZAM YAZINDUA DUKA LAKE LA VIFAA VYA MICHEZO JIJINI DAR

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akkata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la vifaa vya michezo lililopo Kariakoo,Mtaa wa Swahili na Mkunguni jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akioneshwa moja ya mashine ya kisasa iliyomo dukani hapo kwa ajili ya kubandika namba pamoja majina kwenye jezi za washabiki ama wapenzi wa timu hiyo iwapo watapenda kufanya hivyo kwa gharama iliyo nafuu kabisa.
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo la uzinduzi wa duka la vifaa vya michezo lililopo Kariakoo,Mtaa wa Swahili na Mkunguni jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi

Moja ya jezi "uzi" ukioneshwa mbele ya wana habari hawapo pichani

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akioneshwa baadhi ya jezi mbalimbali za timu hiyo zinazopatikana dukani humo maalum kwa mashabiki na wapenzi wa soka.

Na Bakari Issa Madjeshi

Klabu ya Soka ya Azam leo imezindua rasmi duka lake la vifaa vya michezo lililopo Kariakoo,Mtaa wa Swahili na Mkunguni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya uzinduzi wa duka hilo,Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo,Saad Kawemba amesema duka hilo linauza vifaa mbalimbali vya michezo vya timu hiyo na kuuzwa kwa watu mbalimbali.Pia amesema wanatoa nafasi kwa Wanachama wa Klabu hiyo kuwa vifaa hivyo vinapatikana dukani hapo pamoja na kuzingatia familia za Wanachama hao ikiwemo kupatikana Mabegi ya shule kwa watoto wao.

Ameeleza kuwa kwa wale walio nje ya mkoa wa Dar es Salaam watawasiliana na Tovuti(Website) ya Azam pamoja na Mitandao ya kijamii ikiwemo ‘Facebook’.Kawemba amewaomba Wanachama wa Klabu hiyo kujitokeza kununua vifaa hivyo ikiwa ni pamoja na maandalizi ya mechi ya kesho baina ya Azam FC dhidi ya Dar es Salaam Young Africans,mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho utakaopigwa dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Kuhusu maandalizi ya Mchezo wa Kesho wa Fainali baina yao na Yanga,Kawemba amesema wamejiandaa vyakutosha na watahakikisha wananyakua ubingwa wa Kombe hilo ambalo linadhaminiwa na wenyewe Azam. 
Post a Comment