Saturday, May 21, 2016

NEYO APOKELEWA KAMA MFALME JIJINI MWANZA

Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jioni hii akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kupiga ‘Live Music’ katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini, Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama, Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.
Neyo check out from the hotel Hyatt RegencyMsanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akiondoka katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza kwenye Jembeka Festival 2016 ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM. Kulia ni Meneja wa Hoteli hiyo, Timothy Mlay.
IMG_5465
Attu Mynah and NeyoMeneja Masoko wa CFAO Motors Group, Attu Mynah ambao wamedhamini usafiri uliotumika kumwendesha msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo gari aina Mercedes Benz GLE 350 D ya mwaka 2016 katika picha ya kumbukumbu na Msanii huyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Neyo ta Hyatt Regency-The Kilimanjaro
Msanii wa kimataifa Neyo aki-show love na walinzi maalum kabla ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari ya Mwanza.
Neyo official car Mercedes Benz GLE 350 D of 2016
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum aina ya Mercedes Benz GLE 350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO Motors Group.
Neyo Sorrounded by Tanzanian BodyguardMsanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere akiwa amezungukwa na walinzi maalum alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
Neyo at Julius Nyerere International AirportMsanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mlinzi wake wakielekea jijini Mwanza leo jioni.
Costantine Magavilla and NeyoMwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (t-shirt ya blue) na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakijianda kupanda ndege ya Shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea jijini Mwanza. Shirika la Ndege la Fastjet ni miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo.
Neyo Crew to MwanzaMkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akiwa na ‘crew’ iliyoambatana na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakipanda ndani ya ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza

No comments: