Friday, May 13, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AONDOKA KAMPALA KUREJEA NCHINI TANZANIA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na baadhi ya  viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa Viongozi wakuu wanchi mbalimbali siku walipowasili Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kikundi cha ngoma za asili cha Entebe nchini Uganda wakati akiondoka kurejea nchini.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita mbele ya gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga katika uwanja wa ndege wa Entebe wakati akiondoka kurejea nyumbani Tanzania.



Waandishi mbalimbali wa Habari kutoa nchi tofauti wakiwa na shauku ya kupata picha ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni zilizofanyika kwenyeuwanja wa Uhuru wa  Kololo, Kampala nchini Uganda. Katika Picha hiyo Rais Dkt. Magufuli alikuwa akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Picha na IKULU.

No comments:

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...