UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE, (JNIA), WAPATA SHIRIKA LINGINE LA NDEGE, NI MAURITIUS AIRLINES

MFANYAKAZI wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, akiielekeza ndege ya Shirika la Ndege Mauritius Airlines, kuegesha kwenye daraja la kushukia abiria (Bridge), kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 6, 2016. Ndege hiyo aina ya Airbus 319 yenye uwezo wa kubeba abiria 130, imetua kwa mara ya kwanza na itakuwa ikifanya safari zake kila Ijumaa ikiruka moja kwa moja kutoka Mauritius kuja Dar es Salaam kasha Nairobi, nchini Kenya.
Magari ya zimamoto yakiipokea ndege hiyo kwa kuimwagia maji ikiwa ni ishara ya ukaribisho

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, JNIA

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, kupitia uwanja wake wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, imeongeza idadi ya mashirika ya ndege yanayotumia uwanja huo baada ya ndege ya kwanza ya Shirika la Ndege la Mauritius (Mauritus Airlines), kutua kwenye uwanja huo jana Mei 6, 2016.

Ndege hiyo aina ya Boeng Airbus 319, yenye kubeba abiria 130, ilitua kwenye uwanja huo majira ya saa 5;20 asubuhi ambapo kama ilivyoada ya kupokea ndege mpya inayoanza shughuli zake kwenye uwanja huo, magari mawili ya zimamoto yalipiga (saluti), kumwagilia maji ndege hiyo wakati ikielekea kuegesha kwenye daraja la kushukia abiria.

Kwa mujibu wa maafisa wa Shirika hilo, ndege hiyo itakuwa ikiruka kutoka Mauritius moja kwa moja na kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo itashusha abiria na kuelekea uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.“Safari ya kutoka Mauritius kuja Dar es Slaam ni kiasi ya masaa matatu .”alisema rubani mkuu wa ndege hiyo, Parikshant Nundlol

Maafisa wa TAA waliiambia K-VIS MEDIA kuwa ndege hiyo itakuwa ikifanya safari yake mara moja kwa wiki kila siku ya Ijumaa.

Rubani mkuu wa ndege hiyo, Parikshany Nundlol, akizungumza na waandishi wa habari wa Mauritius waliofuatana na ndege hiyo

Warembo wa Kitanzania walioshiriki kuipokea ndege hiyo

Comments