MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA RIPOTI YATOLEO LA NANE LA UCHUMI TANZANIA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye uzinduzi wa ripoti ya Toleo la nane 8 kuhusu hali ya Uchumi Tanzania uliofanyika leo tarehe 20/5/2016 katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Makamu wa Rais picha hayupo wakati wa uznduzi wa ripoti ya toleo la nane 8 kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania uliofanyika leo tarehe 20/05/2016 .kwenye hotel ya Hyatt Begency jijini Dar es salaam.[Picha na OMR]
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia Madame Bella Bird baada ya uzinduzi wa ripoti yatoleo la nane 8kuhusu hali ya uchumi Tanzania.
Serikali imesisitiza azma yake ya kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuiwezesha sekta binafsi kuchangia kikamilifu katila maendeleo ya Taifa.Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo kwenye uzinduzi wa ripoti ya toleo la nane la hali ya uchumi Tanzania uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam.
Hali ya uchumi Tanzania ni ripoti inayochapishwa na Benki ya Dunia mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kukuza mjadala wa sera unaojengeka baina ya wadau na watunga sera na kuchochea mdahalo kwenye masuala muhimu ya uchumi nchini.Makamu wa Rais alisema Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kuendeleza nchi lakini katika baadhi ya miradi na hasa ile mikubwa mambo hayakuwa yanaenda vizuri kutokana na ukosefu wa fedha.
"Dunia ilivyo sasa, tutapata fedha, tena nyingi kutoka sekta binafsi. Sasa kuna haja ya kurekebisha sheria zetu, sera na matamko mbalimbali ili kuiingiza sekta binafsi," alisema Mheshimiwa Samia.Alisema Serikali imeona kushirikiana na sekta binafsi kupitia mpango wa ubia baina ya sekta za umma na binafsi (PPPs) ndiyo njia pekee ya kuiwezesha Tanzania kupiga hatua ya maendeleo.
Alibainisha kwamba katika uzinduzi huo wajumbe wametafakari pia umuhimu wa kuwaingiza wazalishaji na hasa wakulima wadogo na wakubwa kama sehemu ya ubia wa maendeleo ya Tanzania.
Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo kuelezea jitihada za serikali katika kukusanya kodi, kupunguza rushwa na kuimarisha nidhamu katika matumizi ya serikali na kusema hatua hizo zimezaa matunda huku makusanyo ya mapato ya kodi kwa kila mwezi yakivuka lengo tangu Disemba, mwaka jana.
Mapema, akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird alisifia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kiwango cha asilimia 7 kwa mwaka 2014 na 2015 ukilinganisha na wa Afrika kwa ujumla ambao umeshuka toka asilimia 4.8 mwaka 2014 hadi asilimia 3.2 mwaka 2015.
Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli kwa kupambana na rushwa, ufisadi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi ambao umeiongezea heshima serikali ndani na nje ya nchi.Bella alisema wakati Tanzania inaelekea kwenye uchumi wa kati serikali inapaswa kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi (PPPs) kwa ajili ya uwekezaji.
 
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es salaam
20/5/2016

Comments