Friday, February 21, 2014

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA JOB MASIMA AKAMILISHA ZIARA YAKE KWA KISHINDO MKOANI RUKWA

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kukagua gari aina ya Ashok Leyland iliyotolewa na Wizara yake kwa ajili kuimarisha viteule vya kijeshi vya Kasanga na Kirando Mkoani Rukwa. Katika kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinavikabili vitua hivyo Wizara ya ulinzi kupitia kwa Katibu Mkuu huyo imetoa gari mbili, boti mbili na fedha Tsh. Milioni 150 kwa ajili ya kuboresha makazi na miundombinu katika viteule hivyo. Kwa upande mwingine amesema kuwa baadhi ya vifaa vingine vitatoka makao makuu ya jeshi katika kuboresha viteule hivyo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akimkabidhi funguo ya gari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kama ishara ya makabidhiano ya gari mbili pamoja na michango mingine itakayotumika katika viteule vya jeshi vya Kasanga na Kirando Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwasha gari hilo kama ishara ya kupokea misaada hiyo kwa viteule viwili vya Kirando na Kasanga vilivyopo Mkoani Rukwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima wa pili kushoto akitoa majumuisho ya ziara yake kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa leo. Katika majumuisho yake pamoja na mambo mengine aliongeza kuwa mchakato wa kupanua kiteule cha Kasanga utawekwa kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha ili kukiongezea ufanisi zaidi. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambae ndiye chachu kubwa ya mafanikio haya kwa kumualika Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi kuja kujionea changamoto zilizopo amemshukuru kwa kuitikia wito wake na mchango wa ujumla uliotolewa na Wizara yake katika kuimarisha ulinzi katika ukanda wa ziwa Tanganyika unaopakana na nchi za Burundi, Zambia na DRC. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu  Symthies Pangisa kushoto  akizungumza katika kikao hicho cha majumuisho ambapo amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na msafara wake kwa kazi nzuri waliyoifanya Mkoani Rukwa katika kipindi chote cha ziara yake ya siku tatu.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao hicho cha majumuisho wakifuatilia kwa makini.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

No comments: