Tuesday, February 18, 2014

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA MPYA YA AIRTEL MONEY

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel money ijulikanayo kama Hatoki Mtu Hapa  ambapo wateja watapa vifurushi vya BURE Packs vya kutuma pesa bure kwa wiki au Mwezi. Halfa ya huduma hii ilifanyika katika Makao makuu ya Airtel Leo

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akionyesha kwa waandishi habari kipeperushi cha huduma ya Hatoki mtu hapa wakati wa…
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel money ijulikanayo kama Hatoki Mtu Hapa  ambapo wateja watapa vifurushi vya BURE Packs vya kutuma pesa bure kwa wiki au Mwezi. Halfa ya huduma hii ilifanyika katika Makao makuu ya Airtel Leo
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akionyesha kwa waandishi habari kipeperushi cha huduma ya Hatoki mtu hapa wakati wa uzinduzi,ambapo wateja watapa vifurushi vya BURE Packs vya kutuma pesa bure kwa wiki au Mwezi. Halfa ya huduma hii ilifanyika katika Makao makuu ya Airtel Leo
Press Release Airtel yazindua huduma mpya ya Airtel money  yazindua  ofa ya Bure PacksDar es Salaam Jumatatu , 17 Februari 2014 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza rasmi huduma ya kisasa ya kifedha kupitia huduma ya Airtel Money.  Huduma hiyo mpya ya kibunifu itatoa uzoefu tofauti wa huduma za fedha kwa wateja wake.Akiongea wakati wa uzinduzi , Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwana  Sunil Colaso alisema "leo tunayofuraha kuzindua huduma  yetu mpya ya Airtel Money ijulikanayo kama  "Hatoki Mtu Hapa", kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wateja wa Airtel watafurahia kufanya miamala bure bila kikoma kwa kununua kifurushi cha Bure Pack  cha  wiki au cha mwenzi."
Vifurushi vya Bure Packs vitawapa  wateja wa Airtel Money uhuru wa kuchagua kifurushi kinachokidhi mahitaji yao  na kuwawezesha kufanya miamala bure bila kikomo kwa wiki au kwa mwenzi kulingana na matakwa yao. Tumezindua huduma hii ili kuwapatia wateja wetu ubora, urahisi na unafuu katika kufanya miamala ya pesa.Kwa wateja ambao hawatajiunga na virufushi vya Bure Pack bado wataweza kufanya miamala ya pesa kwa bei nafuu kuliko zote  ambapo kwa sasa watatozwa asilimia 50% yaani nusu bei ukilinganisha na gharama zinazotozwa na mitandao mingine.  
Tunauhakika wateja wetu watafaidika sio tu kwa ubora, urahisi na ufanisi wa huduma yetu ya Airtel Money bali kwa kupata huduma zenye viwango nafuu zaidi,  Akiongea kuhusu jinsi ya kupata huduma hiyo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatirce Singano Mallya alisema "kujiunga na "Hatoki Mtu Hapa" packs  wateja watalipia 1500 mara moja  tu na kuendelea kufanya miamala bure bila kimomo kwa wiki nzima, vilevile watakaojiunga kwa mwenzi watalipia shilingi 5000 na kuendelea kufaidi huduma bure kwa mwenzi mzima""kwa ubunifu huu mpya huduma ya Airtel money bado itawawezesha wateja kupata huduma nyingine za ziada.
Sasa wateja  wa Airtel Money wanaweza kununua vifurushi vya Airtel Yatosha kwa namba zao  au kwa namba ya mtu mwingine mahali popote , wakati wowote kupitia huduma ya Airtel money," aliongeza. Huduma ya  "Hatoki Mtu Hapa" ni kwa wateja wote wa Airtel nchini , na kwa wateja wapya watakachotakiwa kufanya ni kutembelea Ofisi za Airtel au mawakala wa Airtel Money zaidi ya 35,000 walioko nchi nzima  na kununua simcard mpya kisha kujisajili wakiwa na kitambulisho rasmi na kufurahia huduma. 
Huduma ya Airtel Money imesaidia kuondoa changamoto za huduma za kibenki vijijini na mijini ambapo imewawezesha wateja kutuma na kupokea pesa bure, kulipia Ankara mbalimbali kama ada za shule, Visa ya US, bili ya maji DAWASCO, Umeme LUKU pamoja na DSTV.   Ili kujiunga na huduma ya Airtel Money, Mteja anatakiwa kupiga *150*60#  na kupata Menu ya Airtel Money. 

No comments: