Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiaano wa Kimataifa,Bernard Membe Alipokutana Kwa Mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiaano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada, Mhe. Christian Paradis walipokutana kwa mazungumzo rasmi katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb.). Mhe. Paradis alifanya ziara hapa nchi hivi karibuni kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanazania na Canada.
 Mhe. Membe katika mazungumzo na Mhe. Paradis.
 Mhe. Membe na Mhe. Mkuya na wajumbe wengine wakati wa mazungumzo na Mhe. Paradis (hayupo pichani) . Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu.
 Mhe. Paradis na Ujumbe wake akiwemo Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Alexandre Leveque (wa nne kutoka kushoto) wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mhe. Mkuya akiagana na Mhe. Paradis mara baada ya mazungumzo huku Mhe. Membe akishuhudia.Picha na Reginald Kisaka

Comments