Sunday, February 23, 2014

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Akutana Kwa Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Nabil Fahmy

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mhe. Nabil Fahmy  wakizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu  ziara ya siku tatu ya Mhe. Fahmy hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 23 Februari, 2014. Mhe. Fahmy yupo nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za afya, elimu, uwekezaji na siasa.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Nabil  Fahmy (hayupo pichani) katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) Jijini Dar es Salaam. Mhe. Fahmy yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 21 hadi 23 Februari, 2014. Wakati wa mazungumzo hayo masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za elimu, afya na uwekezaji. Kulia kwa Mhe. Membe ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana.
 Mhe. Fahmy akieleza jambo wakati wa mazungumzo.
  Mhe. Fahmy nae akizungumza wakati wa mkutano huo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana (kushoto waliokaa)  na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga wakinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Fahmy (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao na Waandishi wa Habari.
  Mhe. Fahmy (wa nne kutoka kushoto) kwa pamoja na ujumbe wake  wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mkutano wao.
 Ujumbe wa Tanzania wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Fahmy (hawapo pichani)
 Mhe. Membe akizungumza.
 Mhe. Membe na ujumbe wake wakimsikiliza Mhe. Fahmy (hayupo pichani)
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Fahmy (hawapo pichani).

No comments: