SHIRIKA LA NYUMBA LA
TAIFA
KUHAMA KWA OFISI ZA MAKAO
MAKUU YA SHIRIKA
Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu na umma kwa ujumla kuwa Ofisi za Makao Makuu ya Shirika
la Nyumba la Taifa zimehamia kwenye jengo lake
jipya lililopo Kiwanja Na. 1
kwenye makutano yaBarabara za Ufukoni na Ally Hassan Mwinyi, eneo la Upanga Jijini Dar es salaam.
Aidha, tunapenda kuwaomba wateja wetu wa Dar es Salaam
kwamba wakati Shirika likiendelea kukamilisha zoezi la kuhamisha ofisi zake waendelee
kupata huduma katika ofisi za Mikoa ya Shirika za Ilala, Temeke, Kinondoni na
Upanga.
Utaratibu wa kuhamisha Makao Makuu ya Shirika unafuatia maboresho mbalimbali yanayofanywa na
Shirika tangu mwaka 2010 kama sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka
mitano 2010/15 unaolenga kuboresha huduma kwa wateja na wananchi kwa ujumla.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
Comments