YAENDELEA KONGAMANO LA 9 LA CTO LA MABADILIKO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI (DBSF), MAKAMBA KULIFUNGA ARUSHA
Mkuu wa Huduma za Utangazaji na Mawasiliano ya redio kutoka Shirika la Utangazaji la Kimataifa (ITU), Pham Nhu Hai akiwasilisha mada katika kongamano hilo.
Mjadala ulifautiliwa kwa umakini na washiriki
Maswali na maoni mbalimbali yalitolewa kutoka kwa washiriki wa kongamano hilo la uhamaji wa mfumo wa utangazaji kutoka Analojia kwenda Dijitali.
Mhandisi Mwandamizi wa Utangazaji kutoka TCRA, Andrew Kisaka ambaye aliwasilisha mada juu ya majitaji ya kiufundi katika matumizi ya DVB-T.
Muongozaji wa mjadala huo, Simon Spanswick (kushoto) ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ITU akiwa katika mjadala la na Pham Nhu Hai.
Mkurugenzo Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkoma nae alishiriki kikamilifu katika mijadala mbalimbali ukiwepo ule wa namna gani nchi za Afrika zitaendelea katika kipindi cha miaka 5 - 10 katika sekta ya utangazaji.
Baadae palikuwa na tafrija kidogo ya Cocktail na mambo yalienda vyema kwa mazungumzo ya hapa na pale ya wadau.
Mkurugenzi wa Azam TV nae alikuwepo kufuatilia mijada hiyo na hapa akiwa na wadau wenzake.
Ilikuwa ni bata kwenda mbele kwa washiriki
Burudani hapa ilinoga vilivyo.
Burudani kutoka kwa kundi la kimasai lilikuwepo na kumfanya Katibu Mtendaji wa Shirika la Utangazaji la Jumuia ya Madola (CTO), Tim Unwin kuamua kuchukua taswira zao
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi alikuwa akipita akifuatisha midundo ya Kimasai
Comments