Monday, February 17, 2014

Frank Sanga ameteuliwa kuwa Mhariri Mtendaji Mpya wa Gazeti la Mwananchi

 Frank Sanga 
--
 Idara ya Habari ya Mwananchi Communications Ltd, imetangaza mabadiliko ya Uongozi kutokana na kuondoka kwa baadhi ya waliokuwa wahariri wa gazeti hilo.
 
Katika mabadiliko hayo Frank Sanga ameteuliwa kuwa Mhariri Mtendaji mpya wa Gazeti la Mwananchi akichukua nafasi iliyoachwa na Dennis Msacky. Kabla ya uteuzi huo, Sanga alikuwa Mhariri Mtendaji wa Mwanaspoti, nafasi ambayo imezibwa na Abdul Mohamed.
 
Uteuzi mwingine ni wa Reginald Miruko ambaye anakuwa Mhariri wa Habari (News Editor) wa Mwananchi, akichukua nafasi ya Samson Mfalila ambaye ali-resign mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
Neville C. Meena,
Cell: +255 - 787 - 675555
        +255 - 753 - 555556

No comments:

NHC YAKABIDHI MSAADA KWA WATU WENYE ULEMAVU UBUNGO

  Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kupitia kwa Afisa wake Mkuu wa Habari, Yahya Charahani, limekabidhi msaada wa vifaa vya kusaidia watu we...