Chemba ya Madini na Nishati Tanzania (TCME) imemteua Balozi mstaafu, Bwana Ami Mpungwe kuwa mwenyekiti wake.

Balozi mstaafu, Bwana Ami Mpungwe
-- 

Dar es salaam, 23/02/2014- Chemba ya Madini na Nishati Tanzania (TCME) imemteua Balozi mstaafu, Bwana Ami Mpungwe kuwa mwenyekiti wake. Uteuzi huu wa Bwana Mpungwe kwa mara nyingine, unalenga kujizatiti kikamilifu kwa kuwaleta pamoja washikadau na umma  kushirikiana katika masuala ya sekta ya madini. Pamoja na kuwa Balozi mstaafu na kiongozi mzoefu wa sekta ya madini, Balozi Mpungwe, yupo katika nafasi nzuri ya kuiongoza Chemba kukua kiuongozi katika nafasi yake kama kioo cha sekta ya madini na kuwa kiunganishi cha washikadau wa sekta serikalini, wawekezaji, katika jamii na hata zaidi.

Balozi Mpungwe amesema; “Kwa unyenyekevu mkubwa, ninapokea kazi hii kwa mara nyingine.

Sekta ya madini imeleta faida nyingi sana Tanzania kupitia uingizaji wa Kigeni (Foreign Direct Investment, FDI),  teknolojia ya kisasa, ujuzi wa hali ya juu katika uongozi na utendaji wa uchimbaji wa madini, mabilioni ya shilingi kwa serikali kupitia kodi na fedha za kigeni kila mwaka na kutengeneza ajira nyingi zitokanazo na mchakato mzima wa uzalishaji madini. Kwa kwenda mbele, sisi kama sekta, tumejizatiti katika kutafuta njia bora zaidi za kuwasilisha mafanikio yetu, na pia kusikiliza mawazo ya washikadau wetu katika masuala yanayohusu Taifa letu kwa ujumla. Hii ndiyo dhumuni kuu ya Chemba na mimi nina dhamiria kutoa uongozi wa kina katika kutekeleza lengo hili.

TCME imeongeza nguvu katika jitihada zake za kuuelewesha umma kuhusiana na sekta ya madini na kazi zake  tokea mwaka 2011, kwa mfano, kuanzishwa kwa tovuti mpya ya TCME (www.tcme.or.tz) , uandaaji wa makala yanayohusu sekta ya Madini Tanzania yenye vipengele vinne iliyorushwa kwenye televisheni na pia inayopatikana  katika mtandao wa youtube (www.youtube.com) .  Katika kuboresha zaidi suala la mawasiliano, Chemba hivi karibuni, imemteua Bwana Nyanda Shuli  kuwa  Meneja wa Mawasiliano na Uenezi. Nyanda ni mwenye sifa kubwa ya uendeshaji wa Mawasiliano na Uenezi katika asasi za kijamii.

Uteuzi wa Balozi Mpungwe kuwa Mwenyekiti wa Chemba ya TCME imeleta uzoefu na utaalumu katika nafasi ya uongozi. Balozi Mpungwe ni mwenyekiti wa bodi katika makampuni kadhaa, na ametumikia Taifa kama Mwanadiplomasia kwa zaidi ya miaka 25, na aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania wa kwanza nchini Afrika Kusini.

MWISHO

KUHUSU TCME
Chemba ya Madini na Nishati Tanzania ilianzishwa 1994 na inawakilisha wanachama wake katika sekta ya madini Tanzania.  Huku ikiwa kama sauti ya tasnia hiyo, Chemba hii inachukua nafasi muhimu katika sekta hii kama mpatanishi kati ya jamii ya uwekezaji kwenye madini na wadau muhimu hususan serikali ya Tanzania na umma.

Kwa Taarifa zaidi, wasiliana na:
Nyanda Shuli 

Comments