Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara afungua kikao kazi cha Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano wakati wa Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano unaoendelea mktoani Tanga, ambapo amewataka kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano (hawapo pichani) na kuwataka kuendelea kutumia mitandao ya kijamii katika kuwasiliana na wananchi, wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Mkoani Tanga. kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiteta jambo na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara, wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Leo Mkoani Tanga.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara akiteta jambo na Kaimu Mhariri Mtendaji Mkuu wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel Nderumaki (aliyesimama) wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Mkoani Tanga.Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko na Mwisho ni kulia ni Afisa Mkuu Mawasiliano toka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bw. Peter Millanzi.
Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano waliohudhuria kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano kinachoendelea Mkoani Tanga.
Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano wakiwa kimya kwa ajili ya kuwakumbuka baadhi ya wanataaluma ya habari waliotangualia mbele ya haki, wakati wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Mkoani Tanga.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara akiwa katika picha ya Pamoja na Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakati wa ufunguzi wa wa Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Leo Mkoani Tanga.Kushoto kwa waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene na mwisho kushoto ni Afisa Mkuu Mawasiliano toka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bw. Peter Millanzi. Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko akifuatiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari( MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa na mwisho kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bi. Gaudensia Simwanza.
Comments