Soma Kwa Makini Maoni ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuhusu Mashine za EDF

 Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto Kabwe
---
EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010 kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD, makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni. 

Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs 1,086 bilioni. 

Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63 mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara 16,000.

Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta (Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato inatarajiakukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake iwapo EFD zitatumika.

Wafanyabishara kote nchini wanalalamika. Mwanzoni hoja kubwa ilikuwa ni bei za mashine hizi. Hoja inayoeleweka kabisa. Kamati ya PAC iliwahi kushauri kuwa Wafanyabiashara wapewe bure kabisa mashine hizi (bila kusubiri kurejeshewa kupitia kodi. Kimsingi mashine hizi ni Bure isipokuwa Mfanyabiashara huikopesha TRA na TRA kumrudishia kupitia kodi ya Mapato katika mwaka wa kwanza wa matumizi). 

Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?

Wafanyabiashara wanasema kodi ya VAT ya 18% ni kubwa mno na inakatwa bila kuzingatia manunuzi yao ie gharama zao za uzalishaji. Siku zote VAT inakatwa kutoka kwenye mauzo ghafi au kutoka faida? 

Hebu tujadili masuala haya na yale malalamiko ya msingi yafanyiwe kazi na yasiyo ya msingi yapuuzwe. 
 
Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba.........


Kutoka Ukurasa Wake wa:facebook.com/zittokabwe

Comments