Jeshi la Polisi Wilaya ya Nanyumbu Wamekamata Watuhumiwa wa Usafirishaji wa Meno ya Tembo yenye uzito wa kg 130.6 yenye thamani ya Tshs Milioni 7.35
Mkuu wa Kituo cha Polisi Mangaka Makao makuu ya Wilaya ya Nanyumbu Alfred Mbena akiwa na askari wengine wakiangalia meno ya tembo 58 yenye uzito wa Kg 130.6
Watuhumiwa wa usafirishaji wa Meno ya Tembo ambao wamekamatwa wilayani Nanyumbu Mkoa wa Mtwara yenye uzito wa kg 130.6 yenye thamani ya Tshs Milioni 7.35 katika Hamidu Ngunde (40) wa pili ni Boniphace Msogo (29) na Geddat Mmuni (36) ote wakazi wa Jijini Dar es Salaam wakiwa ndani ya gari la polisi baada ya kumaliza upimaji wa uzito .
Watuhumiwa wa usafirishaji wa Meno ya Tembo ambao wamekamatwa wilayani Nanyumbu Mkoa wa Mtwara wakiwa wanaangalia upimaji uzito wa meno hayo yenye uzito wa kg 130.6 katika ghala lililopo makao makuu ya wilaya hiyo mjini Mangaka kutoka kulia ni Hamidu Ngunde (40) wa pili ni Boniphace Msogo (29) na Geddat Mmuni (36)wote wakazi wa Jijini Dar es Salaam. Picha na Thomas Dominick
Comments