Thursday, February 27, 2014

MAMIA WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA BALOZI KAZAURA JIJINI DAR ES SALAAM


Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alikuwa miongoni mwa maelfu ya waombolezaji waliofika katika ibada ya kuaga mwili wa Balozi, Fulgence Kazaura aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki akiwa katika matibabu nchini India. 
Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mt Peter, Oysterbay jijini, na kuhudhuriwa na viongozi wa chama na Serikali, mabalozi mbalimbali Tanzania waliokuwa wanafanyakazi nje ya nchi kupitia Chama cha Mabalozi Wastaafu (ACTA), wakurugenzi, wanazuoni na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Akizungumza wakati wa ibada hiyo, mtoto wa marehemu, Kamugisha alisema kuwa baba yao alifariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya koo ambayo ilianza kumsumbua tangu mwaka 2012 na iligundulika Juni mwaka jana.
Alisema kuwa baba yao alikuwa akilalamika kushindwa kumeza chakula na baada ya kuhangaika na matibabu katika hospitali mbalimbali nchini, Juni mwaka jana walimpeleka nchini India alikobainika kusumbuliwa na ugonjwa huo.
“Walimtibia na alikuwa anaelekea kupata nafuu kwani walau alirejea katika hali ya kawaida ingawa siyo kama awali” alisema na kuongeza kuwa ilipofika Agosti hali ikabadilika ikabidi wamsafirishe tena nchini India ambako alitibiwa kwa miezi miwili kisha kurudi nchini.
Alisema hali ilibadilika tena Oktoba mwaka jana ndipo akarudishwa nchini India ambako walimfanyia uchunguzi na kugundulika kuwa saratani ilikuwa imesambaa sehemu zingine.
Kwa mujibu wa ratiba ya maziko, mwili wa marehemu utaagwa leo kwenye Ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla ya kusafirishwa kwenda kijiji alichozaliwa cha Igurukati, Bugandika mkoani Kagera kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumamosi.
Kabla ya umauti, Balozi Kazaura aliyezaliwa 11 Septemba,a 1940, alishika nyadhifa mbalimbali kama Ukatibu Mkuu wizara mbalimbali na kuwa balozi wa Tanzania Ulaya (EEC).


Viongozi wa Kanisa hilo la Mt. Peter wakiwaongoza waomboleazaji kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiwaongoza waomboleazaji mbali mbali kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu
Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Prof. Rwekaza Mkandala (mbele) Sir George Kahama,pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya Matibabu
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akimfariji Mjane wa Marehemu pamoja na watoto wakati wa Ibada maalum ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence Kazaura,.
Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.

No comments: