TANGAZO LA KUUZA NYUMBA ZA MFUKO WA PSPF


Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba), Shinyanga (Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele).
Bei za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo.   Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne.
Chini ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na Mkoa ilipo.  Malipo yanaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:
1)                           UNUNUZI KAMA MPANGAJI (HIRE PURCHASE):
Mnunuzi atalipia kwa mpango wa mwezi mmoja mmoja au miezi mitatu kwa mkupuo (installments) kulingana na thamani ya nyumba. Katika mpango huu, mnunuzi anaweza kulipia kutokana na vyanzo vingine vya mapato yake mbali na mshahara wake. Mwanachama wa PSPF aliyechangia chini ya  miaka mitano (5) atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 5,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba na asiye mwanachama wa PSPF atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 10,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba kukidhi vigezo vya kununua nyumba (kama mpangaji).
Mpango huu wa Ununuzi kama Mpangaji (Hire Purchase) utamwezesha mnunuzi kulipa kati ya sh. 450, 000.00 (laki nne na hamsini tu) na sh. 813,000.00 (laki nane na kumi na tatu tu) kwa mwezi kama malipo ya nyumba zinazouzwa na Mfuko kulingana na ukubwa na eneo nyumba ilipo.
2)                           MALIPO YA MARA MOJA (OUTRIGHT PURCHASE)
Mnunuzi atalipia gharama ya kununua nyumba kupitia akaunti ya Mfuko na kisha kusaini makubaliano kabla ya kuhamishiwa umiliki (transfer).
3)                           MKOPO WA NYUMBA KUPITIA BENKI (MORTGAGE BASIS):
Mnunuzi anaweza kuchukua mkopo katika mojawapo ya Benki ambazo Mfuko wa PSPF ina mikataba nazo na kutumia mkopo huo kununulia nyumba. Mabenki hayo ni; CRDB, Azania, Exim na NMB. 
MUHIMU! Iwapo utanunua nyumba kupitia mkopo wa benki (Mortgage) utapaswa kuwa umesajiliwa kwenye Mfuko na kuchangia kwa muda wa miaka mitano au zaidi. Muda wa kurejesha mkopo ni mpaka miaka ishirini na mitano (25) kulingana na matakwa ya Benki husika.
Mwombaji anayehitaji kuona au kukagua nyumba awasiliane nasi kupitia simu: +255 22 2120912/52 au +25522 2127375-6 au E-mail: pspf@pspf-tz.org.
Kwa maelezo zaidi fika Makao Makuu ya PSPF yaliyopo jengo la Golden Jubilee Towers, Barabara ya Ohio au ofisi zetu zilizopo katika kila mkoa.
Imetolewa na 
Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Pensheni wa PSPF 

Comments