Sunday, February 23, 2014

Rais Kikwete aongoza uchangiaji wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili


 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akiwa pamoja na Marais Wastaafu wa Tanzania, Benjamini Mkapa (kushoto) na Mzee Ali hassani Mwinyi wakati wa hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT), Rodrick Kisenge akizungumz wakati wa harambee hiyo ambayo iliandaliwa nao.
 Mlezi wa PAT Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa akizungumza.
 Waalikwa katika hafla hiyo wakifuatilia matukio.
 Mkurugenzi wa Redio One, Deo Rweyunga akitamka kwa niaba ya Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi  ahadi yake.
 Deo Rweyunga akipeana mkono na Rais Jakaya Kwete baada ya kutoa ahadi ya Mengi ya shilingi za kitanzania zaidi ya Milioni 100.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayomboakipeana mkono na Rais Jakaya kiwete baada ya kutoa ahadi ya Mamlaka hiyo.
 Benki ya Posta Tanzania (TTB) nao waliangusha ahadi yao
 Rais Jakaya Kikwete akipokea hundi yenye thamani ya sh. Milioni kumi kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu, wakati wa hafla ya kuchangia maboresho ya matibabu ya watoto katika hospital ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam jana. Katikati ni Rais wa Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT), Rodrick Kisenge na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harison Mwakyembe. Jumla ya shilingi milioni 602 ziliahidiwa.
 Mkurugenzi wa Mfumo wa Mawasiliano wa PPF, Robert Mtendamema akikabidhi mfano wa hundi kwa rais.
Mfano wa kuigwa; Mkurugenzi wa CXC Safaris & Tours, Charles Hamkah, akikabidhi mchango wake.

No comments: