Saturday, February 22, 2014

Mengi asema vyombo vya habari vinapaswa kuwataja kwa majina watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa

Mwenyekiti Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk Reginald Mengi  
---
 Mwenyekiti Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk Reginald Mengi amesema vyombo vya habari vinapaswa kuwataja kwa majina watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa katika taasisi za umma, badala ya kutoa tuhuma za jumla.

Dk Mengi alisema tuhuma za jumla kwamba taasisi fulani ya umma inajihusisha na rushwa, zinawaumiza watumishi waadilifu ambao ni sehemu ya taasisi hizo.
“Mnapotoa tuhuma za jumla kwamba taasisi fulani inanuka rushwa, mnawaumiza wale watumishi waadilifu, tuhuma za aina hiyo zinawaficha wale waovu wanaohusika,” alisema Dk Mengi kwenye hafla aliyoiandaa kuwapongeza wahariri walioshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa ikiwakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea..........

No comments:

🔴🔴TABORA ZOO YAENDELEA KUNG'ARA KAMA KITOVU CHA ELIMU, BURUDANI NA UTALII WA NDANI

Na Mwandishi wetu, Tabora. Bustani ya Wanyamapori Tabora (Tabora Zoo) imeendelea kujipambanua kama kivutio muhimu cha elimu na burudani jiji...