NMB YAENDELEA KUSOGEZA HUDUMA KARIBU ZAIDI KWA WATEJA WAKE‏

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Bw.Meck Sadick (kwanza Kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya hosipitali Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ,Dr Meshack Shimwela .Mashuka ya Hospitali pamoja na Vitanda vya wodi ya akina mama ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa .Makabidhiano haya yamefanyika jana wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB mandela Road Katikati ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw.Salie Mlay.…

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Bw.Meck Sadick (kwanza Kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya hosipitali Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ,Dr Meshack Shimwela .Mashuka ya Hospitali pamoja na Vitanda vya wodi ya akina mama ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa .Makabidhiano haya yamefanyika jana wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB mandela Road Katikati ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw.Salie Mlay.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Bw. Meck Sadick (pili kulia kwenye viti) akiwa kwenye picha ya Pamoja na maafisa wa NMB tawi la Mandela Road.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Bw. Meck Sadick akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mandela Road .Kwanza kushoto ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam ,Bw. Salie Mlay na kwanza kushoto ni  Mkuu  wa kitengo cha Huduma kwa wateja wakubwa  NMB, Bw.Gerald Kamugisha wakishuhudia ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Bw. Meck Sadick akimpongeza Mganga mkuu wa Idara ya Magonjwa ya wanawake na Uzazi Hospitali ya Taifa Muhimbili ,Dr Mathew Kallanga baada ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali vilivyotolewa na Benki ya NMB wakati wa Uzinduzi wa Tawi la NMB Mandela Road  katikati ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam,Bw.Salie Mlay.
Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam,Bw.Salie Mlay akimwelezea jambo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam (kwanza kushoto) ,Bw.Meck Sadick  kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na tawi jipya la NMB mandela Road.
· Vilevile imetoa msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Amana

NMB yazindua tawi jipya barabara ya Mandela mkoani Dar es Salaam.Hili ni tawi la ishirini kufunguliwa katika mkoa wa Dar es Salaaam, na hii inafanya NMB kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania, ikiwa na matawi zaidi ya 500 yaliyosambaa nchi nzima.

Tawi hili la NMB Mandela Road, linatoa huduma mbali mbali za kibenki ikiwemo akaunti za akiba, mikopo  , huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipia kwa niaba  ya serikali na taasisi mbalimbali. Tawi hili litakua wazi kila  Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili  na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi - 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (8:30 asubuhi- 6:30 jioni), Jumapili na siku za sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.

Katika kusherehekea ufunguzi rasmi wa tawi hili, Benki ya NMB ilitoa msaada kwa jamii wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi ili kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi katika kuboresha huduma katika sekta ya afya. Msaada huu unatolewa kwa hospitali ya Amana pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 

Comments