Friday, February 21, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA NNE WA NCHI WASHIRIKI WA KANDA YA KASKAZIN, JIJINI KAMPALA UGANDA

  Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wakiimba wimbo maalumu wa Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Ushirikiano wa Kanda ya Kaskazini, uliofanyika jana kwenye Hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala Uganda, ambapo Tanzania imeshiriki Mkutano huo kama Mwalikwa.
  Rais wa Uganda Yoweri Museven, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa wakuu wa Nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kanda ya Kaskazini. Umoja huo unaundwa na nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na Sudan Kusini,Tanzania na Burundi zimeshiriki mkutano huo kama nchi waalikwa ambao pamoja na mambo megine waliyojadili ni kukamilisha miradi mbalimbali inayofanywa kwa pamoja na ushirikiano huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza katika mkutano huo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) na Rais wa Burundi Gervas Rufykiri, wakitia saini kushiriki katika mkutano huo.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo Ujumbe wa Tanzania.....
  Makamu wa Rais Dkt Bilal (katikati) akizungumza na Rais wa Uganda Yower Museven (kulia) baada ya Mkutano huo.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments: