Monday, February 01, 2016

UNIDO NA CHUO KIKUU CHA MZUMBE WAENDESHA SEMINA KWA WAMILIKI WA VIWANDA VIDOGO VIDOGO VYA UZALISHAJI (SMES) NA WAHITIMU WA VYUO TANZANIA


Mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam Profesa Ganka Nyamsongoro akifunguaSemina kwa ajili ya  wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara na wajasiliamali semina iliyolengaprogramu ya UNIDO wakishirikiana na Chuo kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kupata mafunzo ya ujuzi wa kazi.
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Peacock Hotel Dar
Mshauri wa UNIDO Bw. Mike Laizer akichangia jambo katika semina hiyo
Bw. Deosdadit Bernad Msimamizi wa Programu kutoka UNIDO akielezea kwa undani juu ya Programu  hiyo
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiendelea kufuatilia Semina
 Profesa Prosper Ngowi Msimamizi Mkuu wa Programu hiyo akieleza kwa kina nia na malengo ya wao kufanya hivyo kwa kushirikiana na ‘SMEs’ ili kuwapa ujuzi wa kazi wahitimu na wahitimu kutoa ujuzi wao waliokuwa nao ili kuweza kukuwa zaidi
Wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa wanaendelea kufuatilia semina hiyo kwa makini
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa wanauliza maswali na kuchangia mawazo katika Semina hiyo
Mmoja wa ‘Mentor’ katika programu hiyo Bw. Kaaya akiwa anatoa maelezo kwa wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali jinsi ambavyo watashirikiana katika kuwafundisha kazi wahitimu hao pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali
Picha ya Pamoja kati ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali, Chuo kikuu cha Mzumbe na wawakilishi kutoka UNIDO
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Profesa Ganka akifungua semina fupi na wahitimu kutoka vyuo mbalimbali ambao ni watanzania katika programu iliyo andaliwa na UNIDO ikiratibiwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe juu ya Mafunzo ya kazi ‘Internship’ ambayo yataanza hivi karibuni ambapo wahitimu hao watatakiwa kufanya kazi kwa miezi minne katika viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara  na wajasiliamali
Msimamizi Mkuu wa Programu kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Profesa Prosper Ngowi akiwaelezea wahitimu juu ya Programu hiyo
Baadhi ya wahitimu wakiwa wanauliza maswali na kutaka ufafanuzi katika baadhi ya maeneo ambayo walikuwa hawajayaelewa katika semina hiyo iliyofanyika katika Chuo kikuu cha Mzumbe
Dkt. Darleene Mutalemwa akitoa neno la Shukurani kwa wote wahitimu wote waliofika katika semina hiyo kwa niaba ya UNIDO na Chuo kikuu cha Mzumbe
Wahitimu wakiwa katika semina hiyo ya kupata maelekezo juu ya Programu ambayo inalenga kuwapa Mafunzo ya kazi wahitimu iliyo andaliwa na UNIDO ikiratibiwa na Chuo kikuu cha Mzumbe

No comments: