Wednesday, February 10, 2016

UONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL) LASITISHA HUDUMA YA TRENI YA JIJI MAARUFU KAMA TRENI YA MWAKYEMBE.


Shimo katika tuta la reli  eneo la Buguruni kwa Mnyamani  ambalo limesababishwa na mvua inayoendelea kunyesha hapa nchini ambapo ukarabati wa eneo hilo unaendelea ili kufanikisha usafiri kurejea hapo kesho.


KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya jana Februari 09, 2016. 

Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maji ya mvua kuchimba shimo kubwa katika tuta la reli karibu na stesheni ya Buguruni kwa Mnyamani.

Uharibifu huo uligundulika jana asubuhi mara baada ya treni kupita eneo hilo ikielekea stesheni ya Dar es Salaam.wakati wa safari yake ya kwanza kutoka Kituo cha Ubungo Maziwa.

Tayari mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakiendelea na kazi ya ukarabati na kwamba inatarajiwa huduma hiyo itarejea tena hapo kesho kama kawaida.

Atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenziye.
Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,

Nd Masanja Kungu Kadogosa

Dar es Salaam,

Februari 09, 2016
Post a Comment