Friday, February 19, 2016

DDCA YACHIMBA VISIMA 52 NA MABWAWA 3 SIKU 100 ZA RAIS DKT. MAGUFULI

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa Bw. Egwaga Nungu akiongea na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) na kuwaeleza kuhusu Mafanikio waliyoyapata Katika Siku 100 za uongozi wa Rais John Pombe Magufuli ikiwamo kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu mbalimbali nchini, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Saalam, Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari-MAELEZO Bi. Lilian Lundo.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO


NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA) wamefanikiwa kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu mbalimbali nchini Katika Siku 100 za uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Hayo yamesemwa  na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa Bw. Egwaga Nungu wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

 “Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA) katika kipindi cha kuanzia Novemba hadi februari tumeweza kufanikiwa kuchimba visima 52 zitakavyowezesha kupataikana kwa maji safi kwa watanzania katika maeneo mbalimbali na pia wakala umefanikiwa kuchimba mabwawa 3” Alisema Bw. Egwaga.

Akiongelea Matarajio na mipango ya wakala Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Bw. Egwaga amesema kuwa wakala unatarajia kuchimba visima 400, kupima wingi wa maji katika maeneo 420, kusafisha visima 500, pumping installation visima 400 na kukarabati visima 100.


Katika kipindi cha miaka kumi wakala wamefanikiwa kuongeza cha maji kwa jamii kwa wastani wa 53,823m3 za maji kwa siku na kufikia wastani wa asilimia 86 na kuwawezesha wananchi kupata vyanzo vya maji safi na salama kupitia uchimbaji wa visima.
Post a Comment