Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu Samora jijini Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa kutumia simu orijio ili kuepuka usumbufu utakojitokeza kwa kuzimwa kwa simu feki ifikapo June mwaka huu.
Akizungumza Leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzindizi wa duka jipya la kampuni ya huwawei mkuu wa mkoa bwana said Meck sadiki amesema kuwa zoezi la uzimaji wa simu hizo uzimaji huo haujaanzia hapa nchini bali limefanyika katika nchi nyingi zilizoendelea.
Aidha Meck Sadick amesema kuwa ni wakati sasa wa makampuni ya simu kuakikisha yanatengeneza simu imara na kuwa na mafundi wa uhakika ili kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa wateja wao.
Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya Huawei, ambapo wanajitahidi kuwa Karibu zaidi na wateja wake na kuendeleza zaidi uzoefu katika matumizi ya bidhaa za Huawei.
"Ili kuwahudumia Zaidi wateja wake Huawei tume fungua Maduka Mapya ya Huawei pamoja na huduma za matengenezo ya simu za mkononi jijin Dar es Salaam,baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei na kuhakikisha kuwa na vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.leo jijini Dar es Salaam" amesema Zhangjunliang.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akipatiwa maelekezo na Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu , Samora leo jijini Dar es Salaam.
Comments