Friday, February 19, 2016

MWENYEKITIWA BMT AMTEUA MOHAMED KIGANJA KUWA KATIBUMTENDAJI

Na Lilian Lundo – Maelezo

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Deonis Malinzi amemteua Mohamed Kiganja kuwa Katibu Mtendaji mpya wa baraza hilo baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo Bw. Henry Lihaya kutenguliwa.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti Malinzi ameeleza kuwa uteuzi huo umekuja baada ya kuona mapungufu ya utendaji kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.“Baraza la Michezo Tanzania limefikia maamuzi haya baada ya kutoridhishwa na utendaji wa Bw. Lihaya na hivyo Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kufanya maamuzi ya kumtengua” alisema Bw. Malinzi

Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya BMT namba 12 ya mwaka 1967 kifungu namba 5(1) ambacho kinampa mamlaka Mwenyekiti wa BMT kuteua Katibu Mtendaji baada ya kupata idhini ya Waziri mwenye dhamana.

Aidha kabla ya uteuzi huo Kiganja alikuwani Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka 2015 mpaka uteuzi wake ulivyofanyika.

Pia aliwahi kufanya kazi kama Afisa Mwandamizi Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania na Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi wa Waziri Mkuu, anashahada ya kwanza ya Elimu katika masuala ya Michezo na Utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

No comments: