Bondia Mserbia anayeishi Uingereza, Geard Ajetovic (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile (kushoto) na Promota Jay Msangi (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari jana. Ajetovic atapigana na Francis Cheka Jumamosi kwenye viwanja vya leaders club kuwania mkanda wa uzito wa Super Middle wa Mabara wa chama cha WBF
Bondia Mserbia anayeishi Uingereza, Geard Ajetovic (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana tayari kwa pambano lake la jumamosi dhidhi ya Franci Cheka. kushoto ni Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile na kulia ni promota Jay Msangi. Ajetovic atapigana na Francis Cheka Jumamosi kwenye viwanja vya leaders club kuwania mkanda wa uzito wa Super Middle wa Mabara wa chama cha WBF.
Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile (katikati) akizungumza katika mkutano huo.
………………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Bondia Geard Ajetovic amewasili nchini na kumuita bondia nyota wa ngumi za kulipwa nchini ,Francis “SMG” Cheka kuwa ni ‘babu’ na hawezi kupigwa na bondia huyo pamoja na kupigana katika ardhi ya Tanzania.
Ajetovic alisema kuwa anamjua Cheka kwani amemuona kwenye pambano lake dhidi ya Thomas Mashali na kusema kuwa ‘amekwisha’ na kamwe si bondia wa kupambana naye.
Alisema kuwa Cheka amepigwa na bondia ambaye si lolote wala chochote na atampiga kabla ya raundi ya tano katika pambano hilo la ubingwa wa Mabara la uzito wa Super Middle unaotambuliwa na chama cha WBF.
“Cheka ni babu, si bondia wa kiwango changu, nimemuona na hana chochote kwangu, siwezi kupoteza pambano hili, ni rahisi ndiyo maana nimewahi kufika siku moja kabla ya muda niliopanga kuja hapa,” alisema Ajetovic.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Advanced Security, Juma Ndambile aliwahakikishia mashabiki wa ngumi za kulipwa nchini kuwa maandalizi ya pambano hilo yamekamilika bada ya ujio wa Ajetovic.
Ndambile alisema kuwa maofisa wa Chama cha WBF, ikiwa pamoja na Rais wake, Howard Goldberg na mwamuzi wa pambano hilo ambao watawasili leo.
“Kama nilivyosema hapo awali, dhamira kubwa ya kampuni ya Advanced Security in kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa nchini hasa kwa mabondia kufaidika na vipaji vyao na si vinginevyo,”
“Ili kufikia lengo letu, Advanced Security imeamua kuwashirikisha mabondia chipukizi katika mapambano ya utangulizi. Mabondia hao chipukizi wanatarajia kutoa changamoto kwa mabondia maarufu ambao pia watashiriki katika pambano hilo,” alisema Ndambile.
Alisema kuwa wameandaa mabondia chipukizi ili kupamba siku hiyo. Alisema kuwa Mohamed Bakari atapambana na Cosmas Cheka katika pambano la uzito wa feather la raundi nane (8) huku Mohamed Matumla ataonyeshana kazi na Mustapha Dotto katika pambao la uzito wa Light la raundi nane pia.
Bondia mkongwe na maarufu nchini, Mada Maugo ataingia ulingoni kwa kupambana na bondia kutoka Mbeya, Baraka Mwakansope baadala ya bondia Abdallah “Dulla Mbabe” Pazi kama ilivyotangazwa awali.
Alisema kuwa pia siku hiyo, bondia wa kike, Lulu Kayage atazichapa na bondia nyota kutoka mkoa wa Mbeya, Mwamne Haji katika pambano la uzito wa fly lilillopangwa kuwa la raundi sita.
Comments