WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU ASIMAMISHA WAKURUGENZI WANNE (MSD)

mp1
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akisimamia maandalizi ya wodi mpya ya wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jana. Rais John Magufuli aliamuru jengo lililokuwa likitumiwa kwa huduma za Uzazi na Mtoto kutumiwa kama wodi ya wazazi kuanzia leo.
mp2
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akisimamia maandalizi ya wodi mpya ya wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jana. Rais John Magufuli aliamuru jengo lililokuwa likitumiwa kwa huduma za Uzazi na Mtoto kutumiwa kama wodi ya wazazi kuanzia leo.
mp3
……………………………………………………………………………
 Waziri wa afya maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto ameagiza watumishi wa nne wa MSD waandikiwe barua ya kusimamishwa  kazi  kutokana na kukiuka taratibu za manunuzi.
Watumishi hao ni Mkurugenzi wa Kanda na huduma kwa wateja  Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Joseph Tesha, Mkurugenzi wa Ugavi Misanga Muja pamoja na Mkurugenzi wa manunuzi  Hery Mchunga.
Wakati huohuo watumishi wa Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , jinsia , Wazee na Watoto kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto tayari wametekeleza agjizo la Rais John Magufuli la kuhama katika ofisi hizo ili jengo hilo litumike  kwa ajili ya wazazi.
Juzi Rais Magufuli aliagiza watumishi wa wizara hiyo kitengo cha afya ya uzazi na mtoto kuhama katika jengo hilo ili kupisha Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- ilitumie kama wodi ya wazazi.
Zoezi la kuhama lilianza tangu jana na kuendendela leo asubuhi kwa ushirikiano kati ya Wizara ya afya  na MNH  .
Katika agizo hilo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa –MSD- Laurean Bwanakunu amekabidhi vitanda 120 , madogoro 120 , Vitanda vya kuzalishia 10, vitanda vya watoto njiti 10 pamoja na mashuka 480   vyenye thamani ya Shilingi Milioni 88. 7.
Akipokea vifaa hivyo Waziri Ummy  amemshukuru Rais Magufuli kwa kuonesha  kuguswa na changamoto zinazoikabili sekta aya afya  nchini na kuzitafutia ufumbuzi .
Pamoja na mambo mengine Waziri Ummy  ameagiza kupatiwa taarifa ya hali ya vitanda kila siku katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili pamoja na hospitali nyingine za serikali.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji  wa MNH , Profesa Lawrence  Museru amemhakikishisa Rais Magufuli kwamba hakuna mama mjamzito atakaye lala chini na kueleza kuwa tatizo kubwa lilikua ni nafasi hivyo kutokana na agizo hilo wamepata nafasi itakayochukua vitanda zaidi ya 120 .

Comments