Tuesday, February 23, 2016

MGAMBO WASIO WAADILIFU KUSHUGHULIKIWA

675  mashujaa Mgambo
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Kutokana na tabia ya baadhi ya mgambo katika Halmashauri za Jijini la Dar es Salaam kujipatia fedha kwa njia zisizo za halali, serikali kupitia Halmashauri zake imejipanga kuwachukulia hatua za kisheria migambo wote watakaobainika kujishirikisha na vitendo vya rushwa.
Akitoa ufafanuzi juu ya madai ya wanachi juu ya mgambo wanaochukua rushwa nje ya faini halali zinazistahili kutozwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Ilala, Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shabibu amesema kuwa zipo baadhi ya taarifa wamepewa na watawachukulia hatua kwa kuwasitishia mikataba wale wote watakaobainika kukiuka sheria na taratibu za kazi.
“ Wapo mgambo ambao watumia vitambulisho feki na kufanya vitendo vya rushwa bado hatujawakamata ila  hatutawafumbia macho tutawachukulia hatua kali za kisheria kwa yoyote atakayekamatwa akipokea rushwa na hata wale watakaotoa rushwa”
“Napenda kuwaasa watanzania kuacha kuwapa fedha mgambo ili kukwepa kulipa faini halali hivyo basi nawaasa watu kutii Sheria bila shuruti kama umefanya kosa kwa mujibu wa Sheria lipa faini kwa mujibu wa Sheria lipa faini halali ili tuondoe vitendo vya rushwa na kuiongezea mapato Serikali ”Alisema Tabu.
Afisa Tabu amewaomba watanzania kutoa taarifa za mgambo wote wanaopokea rushwa na kusisitiza kuwa tabia hii inayoendelea ikome mara moja na mgambo wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa watasitishiwa mikataba yao ya kazi kwa kukiuka maadili ya kazi zao
.
Mgambo katika Jiji la Dar es Salaam wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuchukua rushwa kuanzia shilingi 5,000/= mpaka 10,000/= badala ya kutoza faini ya shilling 50,000/= inayostahili kutoza kwa wale wanaokiuka kanuni na taratibu za afya na mazingira katika Halmashauri mbalimbali.
Katika kupambana na suala la mgambo wasio waadilifu,Halmashauri zimejipanga kuwaajiri vijana walipitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliopata mafunzo yenye yenye kujenga uadili na uwajibikaji katika kazi ili kudhibiti suala la mmomonyoko wa maadili na utendaji kazi mbovu wa mgambo katika Halmashauri mbalimbali. 
Post a Comment