Thursday, February 18, 2016

WAZIRI KITWANGA AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI, AWATAKA WAPANGE MIKAKATI MIPYA YA KUPAMBANA NA WAHALIFU NCHINI

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Polisi nchini kabla ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Jeshi hilo, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kutoka Mikoa yote nchini kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. Watatu kulia meza kuu ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akitoa hotuba yake kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi lake, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) kuzungumza na maafisa hao kutoka mikoa yote nchini na kuufungua Mkutano wao wa Mwaka unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga kabla ya kufungua mkutano huo, aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB nchini, Ineke Bussemaker, mara baada ya kumkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia), Shilingi Milioni 75 kwa ajili ya kuudhamini Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa yote nchini. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Kitwanga katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, na aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini.
Post a Comment