WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUKAGUA

Tazama video ya tukio hilo hapa:
muhimbili waziri wa afya
Dk.Stanslaus Ntiyakunze (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha mawaziri namna jengo linavyokarabatiwa ikiwemo miundombinu yake inavyotakiwa kuwa pindi litakapokamilika ikiwemo suala la mfumo wa maji safi na maji taka. Kuliwa kwake ni Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwangalla wengine Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo ya Muhimbili, Prof. Laurance Masaru (kushoto) na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu (katikati).

Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli wameendelea kufanya kile ambacho wananchi wanataka ikiwemo suala la kutumikia wananchi ambapo mapema leo, Februari 17, Mawaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dk. Hamisi Kigwangalla wameweza kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kukagua majengo likiwemo lile aliloagiza Rais kuwa litumike kuwa wodi ya akina mama.

Mawaziri hao wamefika Hospitali hiyo ya Taifa majira ya mchana na kisha kupokelewa na wenyeji wao akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Prof. Laurance Masaru na kisha kukagua moja ya majengo lililopo jengo la watoto ilikuona namna ya kuweza kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali hyo ya Taifa.

Mbali na kukagua majengo pia walipata kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji ikiwemo wodi maalum ya wagonjwa wa figo, wodi ya akina mama, wodi ya watoto na upasuaji mdogo pamoja na wodi ya watoto wa ugonjwa wa moyo na ile ya watoto wa ugonjwa wa kansa.

Aidha, Waziri Ummy Mwalimu ameeleza kuwa jengo ambalo Rais ameliagiza litumike kama wodi ya akina mama, amebainisha kuwa agizo hilo wameweza kulitekeleza ndani ya siku moja na awali wamefanikiwa kulaza wagonjwa zaidi ya 40 na hadi kufikia leo wameweza kufikisha wagonjwa 53.

Hata hivyo, Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi na vyombo vya habari kuwa wavumilivu kwa kipindi cha sasa kwani tayari ukarabati unaendelea kuakikisha miundombinu inawekwa sawa na ndani ya wiki moja itakuwa imekamilika.

Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog
muhimbili2
Mkurugenzi wa ufundi, Gaudence Aksante akiwaongoza Mawaziri wa Wizara ya Afya kuelekea katika jengo hilo linalofanyiwa ukarabati ililitumike kwa matumizi zaidi ya wagonjwa kuondoa msongamano hospitali hiyo ya Muhimbili.
muhi
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akipata kuwafariji watoto wanaopatiwa matibabu katika wodi maalum ya matibabu ya kansa.
muimbiliWaziri wa Afya akimjulia hali mmoja wa wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika kitengo cha magonjwa maalum ikiwemo Figo. Mgonjwa huyo alipongeza mawaziri hao kwa kuweza kufika hospitalini hapo na kuwajulia hali.
muhimbili33
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati alipotembelea katika wodi ya wagonjwa wa Figo.
muhimbilin77
Waziri Ummy Mwalimu akiwa pamoja na watoto wanaopatiwa matibabu ya ugonjwa wa kansa katika hospitali hiyo ya Muhimbili katika jengo la Watoto.
muhimbili999
Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Muuguzi mkuu Bi. Praxeda Chenya, wengine ni Waziri Ummy Mwalimu wakati wakiondoka katika jengo hilo la watoto mapema leo Februari 17, 2016.
muhimbili
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Laurance Masaru akitoa maelezo namna ya walivyojipanga kuhakikisha wanasaidia wagonjwa wote wanaofika kutibiwa hospitalini hapo. wanaofuata ni Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla na Waziri Ummy Mwalimu pamoja na watendaji wa hospitali hiyo mchana wa leo Februari 17. 

Comments