Sunday, February 07, 2016

RAIS DKT MAGUFULI AZIDI KUWAKOMALIA WATUMISHI WA SERIKALI


Hii ni sehemu ya hotuba fupi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli alipoitoa leo mchana mbele ya Wananchi wa Singida,alipoombwa awasalimie,kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM mkoani Singia

" Leo (jana) sio siku yangu ya kutoa hutuba, ni siku ya bosi wangu, mheshimiwa Mmwenyekiti wetu wa chama cha mapinduzi, chama tawala ambapo sisi viongozi tunatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi. Lakini nataka nichukue nafasi hii chanya ambayo nimepewa niwashukuru wananchi wa Singida na watanzania kwa ujumla kwa kunipa kura nyingi na kuwa Rais wenu. 

Napenda kukuthibitishia mwenyekiti wetu, mimi pamoja na serikali ninayoiongoza tutaendelea kukienzi chama cha mapinduzi na tutatekeleza ilani ya uchaguzi ili wananchi wote waweze kuondolewa kero zao.Kero zote zinazowakabili wananchi tutahakikisha tunazitafutia ufumbuzi wa haraka, lengo likiwa ni kufuta kabisa ndoto za wapinzani kushika dola.

 Na nitoe wito kwa watendaji wote wa serikali, watendaji wote wa serikali kuanzia juu mpaka chini, anaejijua ni mtendaji wa serikali ana jukumu moja tu la kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi. 

Asieweza atupishe pembeni, uwe mkuu wa wilaya, tekeleza ilani ya CCM, uwe katibu tarafa, wewe uko ndani ya CCM kwa sababu tunaoteua ni sisi, mimi ni Rais lakini ni Rais niliechaguliwa na chama cha mapinduzi. Kwa hio nitoe wito kwa watendaji wa serikali ambao wanapokuwa kule wanajifanya wao ni watendaji wa serikali, wajue serikali hii inaongozwa na Rais mwana CCM ambae yuko hapa kwa ajili ya kutekeleza. 

Nilitaka hili niliweke wazi, tumedhamiria kufanya kazi na ninasema tutafanya kazi kwelikweli na ndio maana kauli yetu ni hapa kazi tu, lakini pia imeungwa mkono na chama changu na mheshimiwa mwenyekiti kwamba kazi ipo pale" .

No comments: