Tuesday, August 04, 2015

Mkutano Mkuu Chadema 2015 Wampitisha Lowassa na Juma Dunia hadi kuwakilisha Ukawa






Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zanzibar, Salum Mwalim amemshukuru Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kwa kumsajili Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Salim, amesema “Usajili uliofanywa na Mbowe wakati wa dakika za mwisho unastahili pongezi kwani wanaenda kushinda kwa kishindo.”
Mwalimu ameyasema hayo leo katika Mkutano Mkuu wa chama hicho unaoendelea muda huu katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Naye mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati akihutubia mkutano huo amesema Tanzania ina ndoto ya mabadiliko ambayo inachagizwa na kazi kubwa iliyofanywa na viongozi na wanachama wa Chadema wakiwemo CUF, NLD na NCCR-Mageuzi.
“Tunapopigania ndoto ya Taifa lazima tukubali kuwa umoja wetu usiotenganishwa kwa misingi ya kikabila wala misingi ya udini, tunawahitaji Watanzania wote ili kwa pamoja tutekeleze ndoto ya mabadiliko katika nchi yetu”
Mbowe, anasema anaimani wameanza na Mungu na watamaliza na Mungu na katika utendaji wa miujiza anatenda kwa ajili ya chama hicho kwa makusudi na siyo kwa bahati mbaya ili kulijenga taifa.
Anasema ili Taifa lipate mabadiliko ya kweli, kila mmoja aungane na UKAWA ili kulijenga taifa.
Mbowe, anasema ushirika wao una maana kama walivyokubaliana kwenye UKAWA kwamba wawe na mgombea mmoja wa urais katika mchakato huo na kwenye udiwani ili kuwepo na usawa.

CHADEMA: Vigogo wa CCM: Mgana Msindai, Makongoro Mahanga, Ole Medeye, Isaya Bukakiye wamejiunga na Chadema na kukabidhiwa kadi leo katika Mkutano Mkuu, Dar.

No comments: