Wednesday, April 01, 2015

ALI KIBA AAHIDI KUWACHEKETUA MASHABIKI WAKE DAR LIVE

Msanii wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ (katikati) akielezea alivyojipanga kutoa burudani ya nguvu katika shoo yake ya Mwana Dar Live itakayofanyika Sikukuu ya Pasaka ndani ya Dar Live. Kulia ni MC Darada na Msaga Sumu (kushoto).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Onpoint Solution ambao ni wakala wa promosheni wa Kinywaji cha Vita Malt, Bahati Sindi (katikati) akipozi na mwanamuziki Msaga Sumu (kulia) na Kiongozi wa Kundi la Sarakasi la Masai Warriors, MC Darada (kushoto).
Wasanii watakaotumbuiza kwenye shoo ya Mwana Dar Live Sikukuu ya Pasaka wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini sambamba na waandaaji wa shoo hiyo.
Mratibu wa Burudani katika Ukumbi wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ (wa pili kulia) akielezea walivyojipanga kuwapa raha mashabiki wa burudani katika shoo hiyo. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Onpoint Solution ambao ni wakala wa promosheni wa Kinywaji cha Vita Malt, Bahati Sindi (wa pili kushoto) na Kiongozi wa Kundi la Sarakasi la Masai Warriors, MC Darada (kushoto).
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akielezea jinsi Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamini wakuu wa shoo hiyo walivyojipanga kuipamba shoo ya Mwana Dar Live Sikukuu ya Pasaka ndani ya Dar Live, Mbagala. Katikati ni Abdallah Mrisho na Bahati Sindi (kushoto).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Onpoint Solution ambao ni wakala wa promosheni wa Kinywaji cha Vita Malt, Bahati Sindi (wa kwanza kushoto) akiongea kuhusu udhamini wao katika shoo ya Mwana Dar Live. Katikati ni Mrisho na Matina (kulia).
Bahati Sindi (kushoto) akipozi na Isha Mashauzi (katikati) na Msaga Sumu (kulia).
Kiongozi wa Kundi la Sarakasi la Masai Warriors, MC Darada akielezea kundi lao lilivyojipanga kunogesha shoo ya Mwana Dar Live.
Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kama inavyoonekana.
……………………………………………………..
MSANII wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ ametamka kuwa amejipanga vya kutosha anahakikisha anawapagaiwisha mashabiki wake wataojitokeza katika shoo ya Mwana Dar Live siku ya Sikukuu ya Pasaka, Aprili 5 mwaka huu katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya The Atriums jijini Dar, Kiba alisema amejipanga vya kutosha kuhakikisha anadondosha bonge la burudani kwa mashabiki wake wataokuja katika shoo hiyo ambapo siku hiyo ataupiga wimbo huo wa Chekecha Cheketua kwa kutumia ‘live’ bendi.
“Nawaomba mashabiki wangu waje kwa wingi kwani siku hiyo nimejipanga vya kutosha kuhakikisha napiga shoo kali ambayo itawapagawisha watu wote ambao watakuja ukumbini hapo ambapo nyimbo zote nitaziimba kwa kutumia vyombo vya jukwaani ‘live band’.
Naye Mratibu wa Burudani katika Ukumbi huo wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amewataka mashabiki wote wapenda burudani wasikose kufika katika ukumbi huo siku hiyo ya Sikukuu ya Pasaka kwani watapata furaha ya kufika ukumbini hapo.
Pia, Isha Mashauzi na Mashauzi Classic pamoja na Msaga Sumu na Masai Warriors watanogesha burudani mbalimbali katika siku hiyo wakimsindikiza Ali Kiba.
Shoo ya MWANA DAR LIVE inaletwa kwenu kwa udhamini mkubwa wa VODACOM TANZANIASKYY VODKARED BULLVITA MALTVALEUR BRANDYGRANTS,

No comments: