Tuesday, April 14, 2015

BASI LA KAMPUNI YA GAMET TRANS LAPATA AJALI KIBITI-MKOA WA PWANI

Taarifa zilizoifikia Globu ya Jamii hivi punde kutoka chanzo cha kuaminika,zinaeleza kuwa Basi la kampuni ya GAMET Trans linalofanya safari zake Dar-Lindi-Masasi-Nachingwea limepata ajali maeneo ya Kibiti wilaya ya Rufiji-Utete mkoa wa Pwani baada ya kutaka kumkwepa mtu anayedaiwa kuwa na tatizo la ulemavu wa akili,lakini kwa bahati mbaya likamgonga na kufariki papo hapo,taarifa zaidi zinaeleza kuwa baada ya ajali hiyo basi hilo liliacha njia na kupinduka na kupelekea kifo cha mtu mmoja aliyegongwa na wengine waliokuwemo ndani ya basi hilo (idadi ya abiria haikujulikana mara moja) kujeruhiwa. 

No comments:

RAIS SAMIA APONGEZA MPANGO WA HEIDELBERG MATERIALS KUPANUA UWEKEZAJI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea ujumbe wa Kampuni ya Heidelberg Materials, wazalishaj...