Wednesday, April 15, 2015

WAZIRI NYALANDU AANZA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

 Waziri wa Maiasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Adrehem Meru, wakipata maelekezo kuhusiana na mipaka ya hifadhi ya Taifa ya Saadan kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Saadan, Alhaj Hassan Nguruma (katikati) walipotembelea kutatua mgogoro uliohusu wananchi na hifadhi hiyo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Katibu mkuu wake Adrehem Meru wakiwa katika boti katika mto wami juzi walipotembelea hifadhi hiyo kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mpaka katika ya hifadhi hiyo na wananchi.

 Mhifadhi Mkuu wa Saadan, Alhaj Hassan Nguruma(katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Maiasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Aderehem Meru  kuhusiana na mogoro wa mipaka baina ya hifadhi hiyo na wawekezaji wa shamba linalopakana na hifadhi hiyo. Waziri Nyalandu aliamuru mipaka ya zamani izingatiwe ili kumaliza mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyallandu na Katibu mkuu wake Adrehem Meru wakikagua mto Wami ambao awali ulikuwa mpaka wa Hiadhi ya Saadana na kupanuliwa kitu kilichosababisha kuwapo kwa mgogoro wa muda mrefu wa mipaka. Wazir Nyalandu aliamuru mgogoro huo kumalizwa mara moja kwa kuzingatia mipaka ya zamani.

No comments:

Serikali Yabainisha Maeneo ya Miradi ya Umeme wa Upepo na Jua, Kishapu kuzalisha MW 150

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema Serikali imekwishabainisha na kufanya utafiti wa maeneo mbalimbali yanayofaa kuendelezw...