HOTELI YA KISASA YA SHANGANI HOTEL APARTMENTS YAZINDULIWA RASMI

 Mandhari ya nje ya Hoteli ya Kisasa ya Shangani Hotel Apartments iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego usiku jana mjini Mtwara. Pia ulizinduliwa Mgahawa wa kisasa ambapo wageni waalikwa walifaidi kula chakula cha usiku kilichopikwa na wapishi waliobobea kwa mapishi yenye vionjo vya kila aina.

Wageni wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa hoteli hiyo itakayozidi kuongeza hadhi ya Mji wa Mtwara ni, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara, Seleman Mtalika na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma S. Ally.Pia waliwepo wageni wengine kutoka taasisi mbalimbali pamoja na wafanyabishara. Hoteli hiyo inamilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji Akida Zidikheri.
Akida Zidikheri (kushoto) mmiliki wa Shangani Hotel Apartments na . Said Aboud (kulia)pamoja na Mstahiki Mayor wa Manispaa ya Mtwara, Selemani Mtalika ndani ya mgahawa huo wa kisasa uliopo katika hoteli hiyo.
 Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri wakiwa ndani ya moja ya Apartments pamoja naMkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego (kulia), na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara  Fatma S. Ally (kushoto).

 Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri wakiwa ndani ya moja ya Apartments pamoja naMkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego (kulia),
 Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri akiwaonesha wageni waalikwa sehemu ya kutengenezea mikate (bakery), iliyomo kwenye jiko la mgahawa huo.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara, Seleman Mtalika akimkaribisha mkuu wa Wilaya ili aweze kumkaribisha rasmi Mkuu wa Mkoa ili azungumze na wageni waalikwa.

 Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri akitoa shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria ufunguzi huo.
 Wakipata mlo wa usiku kwenye mgahawa huo, kutoka kushoto ni;Mstahiki Mayor wa
Manispaa ya Mtwara, Selemani Mtalika, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego Mwajuma Mchuka Station Manager wa ATC Mtwarana.

 Wageni waalikwa wakipta chakula cha usiku kwenye mgahawa huo
Ni kula kwa kwenda mbele

Comments