Kulia Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine Gibson A.Kilala akitoa maelezo kwa Waziri wa nishati na madini George Simbachawene hivikaribuni jijini Arusha mara baada ya Waziri huyo kutembelea banda lao katika maonyesho ya nne ya madini na vito yaliyofanyika katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha.
(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Baadhi ya madini
Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine Gibson A.Kilala akimuonyesha Waziri baadhi ya madini yanayopatikana katika kampuni yao
Waziri wa nishati na madini George Simbachawene kushoto akipata maelezo mafupi kutoka kwa mfanyakazi wa Moreshine Bw.William Simba
Waziri wa nishati na madini George Simbachawene akiangalia madini.
Waziri wa nishati na madini George Simbachawene akiangalia baadhi ya madini yanayopatikana katika banda la Moreshine kushoto ni mkurugenzi wa kampuni hiyo Gibson A.Kilala na kulia ni William Simba mfanyakazi wa Moreshine
Bango la Kampuni ya Moreshine.
Mkurugenzi wa kampuni ya madini moreshine ya jijini Dar es saalamu Gibson A.Kilala akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
……………………………………………………..
Changamoto ya Watanzania kutokuvaa vito vya thamani vinavyotengenezwa na mawe mbali mbali yanayopatikana hapa nchini imepelekea madini yakiwamo Tanzanite kukosa soko hapa nchini,Soko la madini haswa tanzanite limekuwa nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa watanzania hawana desturi ya kuvaa madini hayo
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Arusha mkurugenzi wa kampuni ya madini moreshine ya jijini Dar es saalamu Gibson A.Kilala alisema kuwa kutokuwepo kwa utamaduni huo miongoni mwa watanzania kumepelekea soko la madini kupatikana nje ya nchi badala ya hapa nchini ambapo yanapatikana.
Aidha ameiomba serikali kuweza kusajili kampuni ambayo itasaidia kusafirisha madini kama zilizo kampuni nyingine za kusafirishia mizigo hapa nchini kama {DHL)ili kuwawezesha wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao kwa usalama zaidi kama zilivyo nchi za jirani kama Kenya.
Hata hivyo ameiomba serikali kuondoa changamoto ya mipaka kwa wafanyabiashara wa madini kwa kuwaruhusu kufuata madini yalipo badala ya kusubiria brokers hali ambayo inawagharimu muda mwingi lakini pia gharama kuongezeka.
Amesema ni vyema wafanyabiashara wakaruhusiwa kwa leseni zao kufuata madini yalipo ili kuwawezesha kufikia migodini tofauti na sasa ambapo leseni zao haziruhusu kufuata madini yanapopatikana badala yake kusubiria broker wawaletee.
Comments