Tuesday, April 21, 2015

HUAWEI KUSHIRIKIANA NA MATAIFA YA AFRIKA KUBORESHA MAWASILIANO

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa masuala ya Ugunduzi wa Digitali Afrika wa mwaka 2015 'Innovation Africa Digital (IAD) uliyofanyika nchini Zimbabwe ambapo Huawei ikiwa mshiriki iliahidi kushirikiana na nchi za Afrika katika kukuza sekta ya Teknohama. 

KAMPUNI nguli katika sekta ya  teknolojia  ya habari na mawasiliano ya Huawei imeomba uwepo wa ushirikiano baina yake na mataifa ya Afrika hususani katika nyanja za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA).


Kwa mujibu wa Makamu wa Raisi wa kampuni hiyo katika ukanda wa Mashariki na Kusini Bw David Wang, hatua hiyo inalenga kutimiza adhma ya pamoja baina ya kampuni hiyo na mataifa ya Afrika katika kuunganisha bara hilo katika mfumo wa mawasiliano.

“ Ili kufanikisha adhma hii ya kuunganisha bara hili katika mfumo wa mawasiliano, Huawei tunategemea zaidi ushirikiano kutoka kwenye serikali za mataifa ya Afrika,’’ alisema  Bw Wang kwenye Mkutano wa mwaka wa masuala ya uvumbuzi wa digitali (IAD) uliofanyika mjini  Victoria Falls, Zimbabwe hivi karibuni.

Kama mdau maalumu kwenye mkutano huo, kampuni hiyo ilipata fursa ya kuonyesha uvummbuzi wake kwenye masuala ya TEKNOHAMA pamoja na vifaa vyake. Kwa mujibu wa Bw Wang, ili kuenda sambamba na kaulimbiu 'UpatikanajiNafuu’ ya mkutano huo , Huawei  kwa sasa wanatengeneza mtandao wa miundombinu ya mawasiliano, ikiwemo mitandao wa LTE kwa ajili ya taifa laZimbabwe.

Mradi huo unalenga  kuziba pengo la maendeleo ya kidigitali kwa kuongeza eneo linalofikiwa na mtandao wa mawasiliono nchini humo pamoja na huduma kwa bei nafuu. “Lakini pia kwenye hili vipaji vya TEKNOHAMA ni muhimu sana kwa maendeleo ya bara hili. Huawei inajikita zaidi pia kwenye kuandaa vipaji hivi kwenye bara hili.’’ Alisema

Akielezea zaidi Bw Wang alisema mnamo mwezi Oktoba mwaka huu Huawei kwa kushirikiana na Serikali ya Zimbabwe watatekeleza mpango wa kijamii wa kampuni hiyo uitwao “Mbegu kwa ajili ya baadae’ utakaotoa fursa kwa wanafunzi 10 kutoka nchini humo kupata mafunzo ya TEKNOHAMA katika makao makuu ya kampuni hiyo nchini China.

Akizungumza kwenye Mkutano huo, Waziri wa TEKNOHAMA, Posta nahuduma za usafirishaji nchini  Zimbabwe Bw. Supa Mandiwanzira alionyesha kutambua kampuni ya Huawei kama nguli wa masuala ya TEKNOHAMA ulimwenguni na yenye utaalamu na uzoefu kiutandawazi katika kutoa hudumanafuu za masuala ya TEKNOHAMA nchini humo.

Mkutano huo wa siku mbili (kutoka Aprili 14-16)ulihusisha washiriki 500,wakiwamo watunga sera, mashirka simamizi, watoa huduma na watumiaji wa kuu wa TECNOHAMA kutoka Afrika na sehemu nyingine dunia, kwa lengo la kutoa huduma muhimu kwa wanahisa , ili kuboresha mazingira ya teknolijia hiyo na kukuza maendeleo ya sekta hiyo.

No comments: