Sunday, April 26, 2015

BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA AFARIKI KUZIKWA JUMANNE JIJINI DAR


Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), amefariki dunia asubuhi ya leo katika Hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo,  jijini Dar es salaam.  
Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam siku ya Jumanne Aprili 28, 2015 - saa 10 Alasiri baada ya swala. 
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe jirani na TCC Club jijini Dar es salaam. 
Mzee Mbita atakumbukwa Tanzania,  bara zima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni  barani Afrika, hususan utawala kidhalimu wa makaburu  Zimbabwe na  Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa Nelson Mandela.

No comments: