Thursday, April 30, 2015

TIMU YA NYOTA FC YAIBUKA KINARA KOMBE LA NDONDO CUP

Wachezaji wa timu ya Umbrella Garden wakielekea katika lango kupiga mikwaju ya Penalti mara baada ya kutoka sare ya goli 1-1
mchezaji wa Nyota Fc akipiga Penelti katika lango la Umbrela Garden
Naibu Meya wa jiji la Arusha Prosper Msofe akifurahia mashindano ya Ndondo Cup katika Viwanja vya Aicc Jijini Arusha.
.Mashabiki waliojitokeza Uwanjani hapo wakifuatilia meza kuu ambayo haipo Pichani
Mashabiki wa Nyota Fc wakishangilia Ushindi mara baada ya timu yao kuinyuka Umbrella garden magoli 6-5
Mlinda mlango wa timu ya Nyota Fc Hamis maarufu kama Dida akiwa anatizama mpira wavuni.

Ashura Mohamed-Arusha

Timu ya  Soka ya Nyota  Fc imeichapa timu ya Ambrella Garden Fc  kwa  Magoli  Sita kwa Matano na kufanikiwa kuondoka na kombe la Ndondo Cup  Sambamba na Kitita cha Shilingi  Laki  Tano Taslimu  katika fainali za Ndondo Cup zilizofanyika katika viwanja vya Aicc vilivyopo Jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa fainali hizo Naibu meya wa Jiji la Arusha Prosper Msofe alisema kuwa mashindano hayo ya ndondo Cup yamewakutananisha vijana wengi ambao wamepata fursa ya kuonesha vipaji  vyao.

Prosper Msofe alisema kuwa mkoa wa Arusha una sifa nyingi lakini katika upande wa Soka kwa sasa Hakuna timu ambayo ipo imara ambao inafanya vizuri katika ligi mbali mbali hapa nchini.

Aidha Msofe alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanaibua vipaji zaidi na kutengeneza timu moja ya mkoa Jiji la Arusha limepanga kununua eneo la kiwanja nje ya mji na kutengeneza uwanja bora wa kisasa ambao utawawezesha vijana wanaopenda kandanda mkoani Arusha kupata sehemu za kuonesha vipaji vyao na badae kuchuja vijana 20 ambao wataunda timu moja ambayo itawakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano mbalimbali hapa nchini.

Kwa sasa hatuna maeneo ya wazi na hili ni changamoto kwetu vijana wetu wana vipaji lakini hawana sehemu ya konesha tumepanga kununua viwanja na kuvitengeneza ili tuanzishe mashindano mbalimbali ambayo yatapelekea tuapte timu bora itakayotuwakilisha vizuri mkoa wetu wa arusha alisema Msofe

Kwa upande wake waandaaji wa  Ndondo Cup ambayo ni kampuni ya Tan Communication Media wamiliki wa redio 5, Mathew Philip alisema kuwa lengo la mashindano hayo ya ni kutoa burudani ya soka la Mchangani kwa wakazi wa Jiji la Arusha lakini pia kuwapa vijana nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika mchezo wa soka.

Mathew alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa burdani mbali mbali kwa wakazi wa Jiji la Arusha huku akisema kuwa mkoa wa Arusha kwa muda mrefu hakukuwa na Soka la Mchangani ambalo lina vijana wengi ambao wana vipaji na kuwawezesha kuonesha uwezo wao kwa kuwa sasa mpira ni Ajira.

Timu zilizoshiriki ni Pamoja na Nyota Fc ambao waliibuka washindi,Ambrella Garden ambao walishika nafasi ya Pili na kujinyakulia shilingi laki tatu,F.F.U Oljoro Fc,Njiro Sports,Tanzanite Fc,Red Star Fc,Lemara Boys,

No comments: