BENKI YA EXIM YATANGAZA ONGEZEKO LA ASILIMIA 35 LA FAIDA YA KABLA YA KODI

 Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kutoka kulia) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari  wakati akitoa  taarifa ya mapato ya mwaka 2014 ya benki ya hiyo jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo , Frederick Kanga (wa pili kulia) na Mkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo, George Binde (kushoto) .
 Meneja Mwandamizi utafiti na Uchambuzi wa Biashara wa Benki ya Exim Tanzania,  Joseph Mrawa (wa pili kulia) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari  wakati akitoa  taarifa ya mapato ya mwaka 2014 ya benki hiyo  jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kutoka kulia) Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo , Frederick Kanga (wa pili kulia) na Mkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo, George Binde (kushoto) 
 Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki ya Exim Tanzania, Frederick Kanga (katikati ) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari  wakati akitoa  taarifa ya mapato ya mwaka 2014 ya benki hiyo  jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kutoka kulia) naMkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo,George Binde (kushoto) 

BENKI ya Exim Tanzania imepata ongezeko la faida (kabla ya  kodi) kwa mwaka 2014 la asilimia 35 kufikia shilingi bilioni 24.1 kutoka shilingi bilioni 17.9 kwa mwaka 2013. Benki imeendelea kuwa na mali za shilingi tilioni 1 na kuweza kukuza pato la wenyehisa kwa asilimia 23 kufikia shilingi bilioni 190 ikilinganishwa na shilingi bilioni 154 iliyorekodiwa mwaka Jana.

 "Tunafuraha kubwa kuitangaza kwenu mafanikio makubwa ya kifedha ya mwaka 2014 Desemba,” alisema Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Issa Hamisi, akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam Jana.

Alisema kuwa benki hiyo imefanikiwa kupata faida (baada kodi) kiasi cha sh bilioni 57.3 kutoka sh billion 44.2 iliyopatikana mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la asilimia 30, ikilenga zaidi katika ongezeko la amana zenye gharama nafuu.

Kwa mujibu wa Bw. Hamisi, pia masuala ya ada, kamisheni na mapato ya fedha za kigeni yaliongezeka kwa asilimia 25 hadi kufikia shilingi bilioni 38 kutoka shilingi bilioni 30.4  kwa mwaka uliopita. Ukuaji huu kwa kiasi kikubwa umechangiwa na kasi ya ukuaji katika shughuli ya za biashara za fedha za kigeni, bidhaa za biashara ya fedha na ada kutoka kwenye  utoaji wa huduma  mbadala.

Mali za benki zimekuwa wakati ‘Gross NPA ratio’ ikishuka kutoka asilimia 9.60 kwa mwaka 2013 kufikia asilimia 6.83 mwishoni mwa mwaka uliyolipotiwa.

Benki hiyo pia iliweka mkakati wa miaka mitatu mwanzo kabisa wa mwaka huo 2014 ambao ulilenga kujiongezea soko lake la amana sambamba na kufikia nafasi ya uongozi katika malipo.

Bw. Hamisi aliongeza kuwa benki imeweka mkakati wa kuzidi kujiimarisha na kuimarisha watu wake, shughuli zake pamoja na teknolojia. Alisema benki imeweza kufanyakazi na makampuni bora ya kimataifa katika utoaji ushauri kwenye masuala yajulikanayo kama Enterprise-wide Risk Management, na pia kuweza kurahisisha zaidi ufanyaji wa shughuli zake kwa mwaka huo.

Aidha Bw Hamisi aliongeza kuwa benki imendelea jitihada za kupanua wigo wa huduma zake kwa kuongeza idadi ya matawi mawili kwenye nchi tatu ambazo inatoa huduma zake vikiwemo visiwa vya Comoro na nchini Djibouti.

“Mafanikio haya ni mwangaza tosha katika utendaji wetu wa sasa na siku zijazo….kwa sasa Exim imejenga msingi imara kitu ambacho kinatuhakikishia mafanikio zaidi kwa mwaka huu 2015,’’ aliongeza Bw Hamisi.

Benki imeendelea kujidhatiti katika urejeshaji wa kile ikipatacho toka kwa jamii. Katika mwaka huo benki ilijikita zaidi katika kusaidia taasisi za elimu, hospitali na taasisi nyinginezo.

Comments