Cake maalum iliyoandaliwa kwenye sherehe za uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins kabla ya zoezi la kuwasha mishuma 70 kwenye cake hiyo ikiwa ni uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Mshehereshaji wa sherehe hizo Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins wakiwa wamejumuika na wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye mnuso huo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiwasha nakshi nakshi zilizowekwa kwenye cake maalum ya uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini. Anayemkingia upepo ni walioandaa Cake hiyo kutoka kampuni ya M.E Gift Wraps and Delivery huku Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins naye akijianda kufanya zoezi hilo.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakishiriki kuwasha mishumaa 70 iliyowekwa kwenye cake hiyo.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakikata cake kwa niaba ya wafanyakazi wenzao.
Comments