SITTI TANZANIA FOUNDATION 2015 INAKULETEA – CHOZI LA SITTI

Zilikuwa siku thelathini (haiyumkini kana kwamba ni zilizozidi masaa ya kawaida yazungukapo bila kubaini) zilizojaa majuto, maumivu makali yasiyomithilika wala kuelezeka.  Nilijiuliza kwa nini?  NIlijiona kana kwamba thamani ya utu wangu imetoweka.  Niliomba Mungu usiku na mchana ingali nikishindwa hata maneno wakati wa sala.

Majuto ni mjukuu na ingali ya jana kamwe haiwezi kuwa kesho, achilia mbali ya leo.  Nimeamka kwani natambua kuna maelfu, mamia elfu ama hata mamilioni duniani kote wapitiao makubwa zaidi ya yangu yaliyojiri.
Nimeamua, nimekata shauri, nimesimama, nimefuta chozi, sitaishi kwa kuwaza ikiwa kama ni njonzi;

‘NIMEAMUA KUPAZA SAUTI, NIMEAMUA KUWA SAUTI’.
Haya ni machache latika kitabu chake kipya kikiitwa – Chozi la Sitti……Kwa nini ukose kuwa sehemu ya HISTORIA?

02.05.2015 kuanzia saa moja usiku @Mlimani City Conference Hall…..Pata tiketi yako SASA: 0685 01 07 17

Comments