UTOAJI WA NISHANI ZA KUMBUKUMBU YA MIAKA 50YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano Dk.Mohammed gharib Bilali pamoja na Viongozi wengine wakiwa  katika picha ya pamoja baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Bw.Damian Zefrini Lubuva baada ya kumvalisha  Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha nishani Bw.Aboud Talib Aboud wakati wa hafla ya kutunuku Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu katika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akivalisha Nishani Bw,Mohammed Seif Khatibu wakati wa hafla ya kutunuku  Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu  katika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Comments