RAIS DR. JAKAYA KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MUUNGANO

1
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dr.Jakaya Kikwete akikagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania ulioasisiwa na Wazee wetu Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume mwaka 1964 kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar, Dr. Jakaya kikwete ameongoza maelefu ya watanzania kwenye uwanja wa Taifa katika sherehe za kuadhimisha muungano huo sherehe zilizohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, Vyama vya Siasa, viongozi wa dini na wananchi wageni waalikwa kwa ujumula.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UWANJA WA TAIFA-DAR ES SALAAM)2Rais Jakaya Kikwete akiendelea kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa.345Vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama vikiwa vimejipanga katika gwaride hilo.6Rais Jakaya Kikwete akirejea jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa.7Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa wamesimama kwenye jukwaa kuu kwa ajili ya kumpokea Rais Dr. Jakaya Kikwete.8Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda mara baada ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania.9Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mh. Pandu Ameri Kificho Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mara baara ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania.10Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh, Seif Sharif Hamad mara baada ya kukagua gwaride la Heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania, Kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  Dr. Gaharib Bilal na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik.11Rais Jakaya Kikwete akiakizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein huku Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiwaangalia kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kulia ni Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal.  wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania12Rais Jakaya Kikwete akipokea heshima kutoka Vikosi vya ulinzi na usalana wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.13Mwenyekiti wa Chama cha TLP Taifa na Mbunge wa jimbo la Vunjo Mh. Augustino Lyatonga Mrema akiwa ameungana na wageni wengine waalikwa katika maadhimisho ya sherehe hizo.14Kikosi Cha bendera kikitoa heshima zake Mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dr. Jakaya Kikwete wakati wa maadhimisho hayo. 15Vikosi vya ulinzi na usalama vikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Mh Dr. Jakaya Kikwete.16Kikosi cha Mizinga kikipita na kutoa heshima zake17Kikosi cha wanamaji wanawake kikipita18Kikosi maalum cha walinzi wa viongozi kikipita na kutoa heshima.19Kikosi maalum cha mizinga ya kutungulia ndege kikitoa heshima zake20Kikosi maalum cha Makomandoo kikitoa heshima zake21Kikosi cha makomandoo wana maji kikipita na kutoa heshima.22Kikosi cha FFU kikipita 23Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo.24Baadhi ya viongozi wakiwa katika sherehe hizo.25Wananchi mbalimbali wakiwa katika maadhimisho hayo.

Comments