Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu kilichopo Manispaa ya Ilala,jana jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Maendeleo ya Bidhaa wa DCB Commercial Bank,Bw.Boyd Mwaisame akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Kompyuta katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu kilichopo Manispaa ya Ilala,jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu wakisikiliza kwa makini risala iliyo kuwa ikisomwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana jana Jijini Dar es Salaam.
0 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu kilichopo Manispaa ya Ilala,jana jijini Dar es Salaam.( Picha na Emmanuel Massaka)
Na Bakari Issa,Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo wa Kompyuta kwa Chuo hicho,Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Dkt.Pindi Chana amesema umuhimu wa Vyuo hivi unatokana na lengo la kuanzishwa kwake aambalo ni kutoa maarifa na stadi zitakazowawezesha wananchi kujiajiri,kujitegemea ili kuondokana na ujinga,umaskini na maradhi hatimaye waweze kuchangia kuinua uchumi wa taifa.
Pia,Dkt.Chana amewahasa wazazi kuacha kuwaacha watoto wao kukaa nyumbani bila kujishughulisha na shughuli yeyote pindi wanapomaliza masomo yao na badala yake kuwashughulisha watoto hao ili kujiepuka kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.
Kwa upande wake,Meneja Masoko na Maendeleo ya Bidhaa wa DCB Commercial Bank,Bw.Boyd Mwaisame amesema Benki imekabidhi msaada huo kutokana na kuguswa na matatizo mengi yanayojitokeza katika jamii likiwemo la ukosefu wa vitendea kazi . kwa watoto wenye Ulemavu.
Naye, Mkuu wa Chuo hiko,Bi.Pulcheria M. Ndamgoba ametoa shukrani kwa msaada huo wa Kompyuta katika Chuo hiko na kuahidi kukitumia vizuri katika kutoa elimu chuoni hapo,huko Kiongozi wa Wanafunzi wa Chuo hiko,Ridhwan Omary akitoa msisitizo kwa Benki hiyo kuwasaidia kujengea viwanja vya michezo.
Comments