MASHABIKI WA TAARAB WAJINOMA KWA MUZIKI WA JAHAZI DAR LIVE

Mzee Yusuf akiimba ndani ya Dar Live.
Mashabiki wakiserebuka huku wakiwa na picha ya Mzee Yusuf.
Leila Rashid akipagawisha mashabiki.
Mashabiki wakiserebuka kwa raha zao.
Wanenguaji wa Jahazi wakipozi mbele ya kamera.
Shabiki akimtunza pesa Hadija Yusuf.
Musa Musa akilicharaza gitaa.
Shabiki aliyetaka kuingia bure ukumbini baada ya kutaitiwa na walinzi.
Fatma Kassim akiimba.
MASHABIKI wa taarab nchini jana walipata walichokitaka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani  wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.
Katika onyesho la jana, Kundi la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf lilimwaga burudani ya nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki kibao waliofurika katika ukumbi huo ambao una kila aina ya ‘mafuraha’ ikiwa ni pamoja na makulaji na vinywaji licha ya hali ya hewa kujenga tishio la mvua kila mara.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL) 

Comments