Aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Kata ya Makuyuni, Badi Mandali akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Tanzania Labour Party (TLP) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kata ya Makuyuni, Himo mkoani Kilimanjaro, juzi. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Mrema na mkewe Rose Mrema.
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema akiwa na wanachama wapya wa chama hicho waliotoka NCCR-Mageuzi, CCM na Chadema mara bada ya kuwakabidhi kadi mpya mara baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kata ya Makuyuni, Himo mkoani Kilimanjaro, juzi.
Aliyekuwa Diwani wa Kata Mwika Kusini (TLP), kabla ya kutimuliwa kwa madai ya kukisaliti chama hicho Meja Jesse Makundi akizungumza kuhusiana na tuhuma zinazomkabili wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lole, jimboni Vunjo mkoani Kilimanjaro juzi.Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema akiongoza maandamano ya wakazi wa Kijiji cha Lole, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ikiwa ni sghemeu ya ziara yake jimboni humo juzi.
Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema akiongoza maandamano ya wakazi wa Kijiji cha Lole, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ikiwa ni sghemeu ya ziara yake jimboni humo juzi.
Wanafunzi wa shiule ya sekondari Muungano wakimpokea Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema mara baada ya kuwasili shuleni hapo, Himo Mkoani Kilimanjaro, juzi.
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema akishiriki katika ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Shule ya Wasichana Wenye Vipaji Maalum ya Muungano, Himo Mkoani Kilimanjaro, juzi.
……………………………………………………………….
Mwandishi Wetu,
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema ametangaza mkakati wa kuisambaratisha NCCR-Mageuzi Vunjo kwa kuzindua rasmi kampeni inayoitwa ‘TOKOMEZA MBATIA VUNJO’.
Akizungumza wakati wa mkutano na wanachama wa chama hicho katika Kata ya Makuyuni Himo, kitongoji cha Kiriche, juzi, Mrema alisema operesheni hiyo ina lengo la kuhakikisha jitihada za Mbatia kulitwaa Jimbo hilo hazifanikiwi.
Mrema ambaye alisema operesheni hiyo ni majibu kwa Mbatia ya kauli yake ambaye alitangaza ‘Delete TLP/ Mrema’, alisema mwanasiasa mwenzake huyo anatumia propaganda chafu dhidi yake ikiwa ni pamoja na kudai kazeeka, hafai na hana uwezo wa kuwaongoza Vunjo.
“Mimi kuanza sasa natangaza ‘TOKOMEZA MBATIA VUNJO’ na ninasema nipo fiti, hafi mtu hapa na nina uwezo ninao wa kuendelea kuwaongoza Vunjo kwani nina mtaji wa kutosha wa watu” alisema.
Mrema aliitangaza operesheni hiyo muda mfupi baada ya kuwakabidhi kadi viongozi sita wa NCCR Mageuzi wa Kitongoji cha Kiriche akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Makuyuni, Badi Mandari na wengine 50 kutoka vyama tofauti.
Mbunge huyo alisema kuwa wakati wa kujua mbivu na mbichi ni sasa na kubainisha kuwa kuna wanachama wa TLP ambao walirubuniwa na Mbatia lakini baada ya kuujua ukweli wamerudi katika chama chake.
Mrema ambaye pia alimkabidhi makalavati manne kwa ajili ya ujenzi wa daraja katika kitongoji cha Kiriche, alisema mfuko wa Jimbo hadi sasa umetumia jumla ya shilingi milioni 15.1 kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika Kata hiyo.
Mara baada ya kupokea makalavati hayo, Mandari, alisema wananchi wa eneo hilo vipindi vya mvua wamekuwa wakipata adha kubwa ambayo wakati mwingine imekuwa ikiwafanya wakakosa mawasiliano ya barabara na wenzao wa maeneo vijiji vingine.
Katika hatua nyingine, Mrema alikataa kuwasamehe mbele ya mkutano huo madiwani wawili waliofukuzwa katika chama hicho, Yolanda Lyimo wa Kata ya Kilema Kati na Meja Jesse Makundi wa Mwika Kaskazini.
“Nimesikia maombi yenu ya msamaha, lakini katika chama sikuwafukuza mimi Mrema, bali ni vikao vya chama hivyo suala lenu nalipeleka mbele ya Kamati Kuu lakini akawashauri ili Kamati Kuu iweze kusikiliza maombi yao sharti muondoe kesi mnayodai fidia dhidi yangu na Naibu Katibu Mkuu, Nancy Mrikaria ya shillingi millioni 500” alisema Mrema.
Comments